WILLIAM LUKUVI MBUNGE WA JIMBO LA ISMANI
WILLIAM LUKUVI MBUNGE WA JIMBO LA ISMANI
NA RAYMONDI MINJA IRINGA
MSOMI wa Digri ya uhandisi wa kilomo na mtaalamu wa kilimo cha
umwagiliaji kutoka chuo kikuu cha kilimo Sokoine (SUA)Mhandisi
Sebastiani Kayoyo (39) anetangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika
jimbo la Isimani kwa tiketi ya CCM linaloshikiliwa na Waziri wa
aridhi ,nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi
Akitangaza nia yake hiyo mkoani Iringa juzi Kayoyo alisema kujitosa
katika jimbo hilo ni kuhakikisha maendeleo yakiongezeka kwa kasi na
kutoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wa jimbo hilo.
Kayoyo alisema kuwa siko kwamba mbunge aliyeko madarakani hajafanya
mambo ya msingi ila mbunge huyo ameongoza jimbo hilo kwa miaka mingi
hivyo ni fursa ya hazina kubwa ya vijana walioko ndani ya chama cha
mapinduzi kuweza kushika hatamu katika kusukuma mbele gurudumu la
maendeleo katika nchii hiii
"Mbunge anayeshikiria jimbo ninamheshimu sana na ameweza kufanya
mambo mengi mazuri, hivyo kwa kidemokrasia nina kuwa na Haki ya msingi
kikatiba, nitahakikisha naendeleza mambo ya msingi ambayo bado
hajayatekeleza, hii ni pamoja na kuongeza nguvu kwa wananchi wengi
waliokosa fursa mbalimbali" kayoyo
Kakoyo ambaye kwa sasa ni mwajiriwa wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa
kama muhandisi wa kilimo (Mtaalamu wa zana za kilimoba kilimo cha
umwagiliaji )ni mzaliwa wa kijiji cha Tungamalenda kata ya idodi
tarafa uya idodi iliyopo ndani ya Jimbo hilo la Isimani
Alipoulizwa kuhusiana na hatima ya ajira yake endapo ataukosa ubunge
,”Mimi ni mtumishi wa serekalina ninajua raratibu zote za utumishi
serekali lakini niko tayari kuacha kazi ili kufanyakazi na ndugu zangu
wa Isimani katika kujiletea maendeleo”
Akitaja vipaumbele vyake endapo chama chake kitampa ridha ya
kukimbiza kijiti hicho Kayoyo alisema kuwa ataweka msisitizo katika
swala la afya , kilimo ,maji safi na salama pamoja na swala la
miundombinu ikiwemo Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwa kwa
kuwa jimbo hilo halijawahi kuwa na lami tangu nchii hii ilipopata
uhuru wake
"Nia yangu ni kuona maendeleo ya jimbo hilo yakiongezeka, napenda
kuona wananchi ambao asilimia kubwa ni wakulima wakipata fursa za
kusafirisha mazao yao nje ya jimbo hilo huku vijana nao wakipata
kuwezeshwa, uongozi ni kupokezana kijiti hivyo kijiti hicho
nitakiongoza vizuri na naomba wananchi siku itakapofika ni kutekeleza
wajibu" alisema Kayoyo
Kwa kujitokeza huko kwa Kayoyo kunafanya idadi ya wagombea kutoka
chama cha mapinduzi CCM kufikia wawili akiwemo Mbunge wa jimbo hilo,
Wiliam Lukuvi ambaye bado ameonyesha nia ya kuendelea kuliongoza huku
kwa upande wa chadema mbunge wa viti maamulu Chiku Abwawo pamoja
makamu mwenyekiti wa bavicha Ole Sosopi
Monday, May 25, 2015
KUMEKUCHA JIMBO LA ISMANI LUKUVI APATA MPINZANI
Monday, May 25, 2015
mwangaza wa hbari
No comments
0 comments:
Post a Comment