juliana shonza akiwahutubia wananchi wa mkoa wa iringa
viongozi chama cha mapinduzi wakiwa katika meza wakifuatia mkutano unavyoendele
na fredy mgunda,iringa.
katibu mkuu
wa uvccm taifa afanya ziara ya jimbo la kilolo kwa lengo la kukijenga
chama na kuangalia maendeleoya chama
hicho hasa ngazi vijana lakini akiwa
katika ziara hiyo aliongozana na mwenyeji wake
katibu wa uvccm mkoa wa iringa.
akihutubia
wakati wa mkutano uliofanyika katika kijiji cha kitumbuka kata ya ilole katibu
wa uvccm mkoa wa iringa elisha mwampashi aliwataka wanachama wa chama hicho
kuondoa unyonge dhidi ya wapinzani wake kwa kuwaambia ukweli wananchi juu ya
maendeleo yanayofanywa na chama hicho.
aidha
mwampashe amesema kuwa ifike wakati viongizi wa chama hicho kuacha kujidanganya
kwa kuwapa taarifa viongozi za matumaini
juu ya maendeleo ya chama hicho.
“tunatakiwa
tubadilika sasa kwa kuwapa taarifa za ukweli viongozi wetu ili wanapoondoka
wajue nini cha kufanya ili kuondoa
dosari ambazo zinzkuwa zikijitokeza,tuenaelekea kwenye uchaguzi mkuu ambao
utafanyika hapo “alisema mwampashe
kwa upande
wake katibu wa uvccm taifa sixtus
mapunda amewapongeza wananchi na wanachama wa tarafa ya ilole kwa ujumla kwa ushindi walioupata wakati wa serikali za
mitaa ambao unaashilia chama hicho kuendelea kupendwa kata tarafa hiyo.
lakini
mapunda aliwatoa hofu wananchi wa kijiji cha kitumbuka kwa kusema amesikia na
kujionea baadhi ya matatizo yanayoikabili kata ya ilole na kuwaahidi
kuyafikisha kwa mbunge wao na kutafuta njia ya kuyatatua kwa kuwa profesa
petter msola ni msikivu.
“tatizo la
kufikisha nguzo za umeme katika eneo hili ni tatizo dogo ambalo linatatulika
kwa haraka na kuwaahidi wananchi kulifanyia kazi mapema ,suala la barabara
alisema kuwa amejionea yeye mwenyewe kuwa
si nzuri na inahatarisha maisha kwa kuwa pindi mvua itakaponyesha
barabara hiyo itakuwa kama mto”.alisema mapunda.
ALIYEKUWA kada
maarufu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema ) Taifa Juliana
Shonza ambae alijiuzulu na chama hicho na kijiunga na CCM amewataka wakazi wa
jimbo la Iringa mjini kuungana kulipokea jimbo kutoka kwa mbunge Mch Peter Msigwa.
Shonza ametoa kauli
hiyo leo wakati akiwahutubia wakazi wa jimbo la Iringa mjini wakati wa mkutano
wa uzinduzi wa matawi unaofanywa na katibu mkuu wa Uvccm Taifa sixtus Mapunda.
Alisema jimbo la
Iringa mjini ni jimbo ambalo wananchi walichagua mbunge kwa hasira na kuwa
badala ya kutegemea maendeleo wamejikuta wakifanya maandamano yasiyo na kikomo
kila uchwao.
Shonza alisema kuwa
mbunge wa jimbo la Iringa mjini amekuwa ni mtu wa kujipigania mwenyewe kimaisha
badala ya kujishughulisha kuwaletea wananchi maendeleo.
Hivyo alisema ni vema
wananchi wa Iringa mjini kujipanga kwa hafla ya kulipokea jimbo hilo kutoka kwa
mpangaji mbunge Msigwa aliyepanga bila kujua kama kapangishwa hivyo kushindwa
kulipa kodi.
Akielezea juu ya hofu
ya muungano wa vyama vinavyounda katiba ya wananchi (ukawa) alisema kuwa
Chadema ni chama ambachokinataka kupanda kupitia ukawa.
Kwani alisema Chadema
ndio chama kilichokituhumu CUF kuwa ni CCM B na kuwa ni chama cha kishoga
imekuwa leo kuungana
Hivyo kuwataka
watanzania kupima na kutoa maamuzi magumu pindi uchaguzi utakapo fika.
Nae mjumbe wa kamati
ya utekelezaji Uvccm Taifa Secky Kasuga alisema wananchi wa jimbo la Iringa
walianzimisha jimbo hilo na sasa mwenye Nyumba anahitaji Nyumba Yake hivyo
lazima mpangaji kuondoka.
"Tunalazimika
kuchukua Nyumba yetu baada ya mpangaji kushindwa kufagia nyumba"
Katibu mkuu wa UVccm
Taifa Sixtus Mapunda alisema kilio cha maendeleo kwa jimbo la Iringa kimetokana
na mchanganyo uliofanywa na wananchi kwa kumchagua mbunge mrudisha nyuma maendeleo.
Alisema mbunge amekuwa
kikwazo kikubwa kwani bungeni wakati wa vikao vya bajeti yeye anatoka nje ya
bunge na wakati wa vikao vya kupanga shughuli za maendeleo halmashauri yeye
anashiriki kuita maandamano.
" Tunawaombeni
wana Iringa mtusaidie kurejesha jimbo kwa kumtoa mbunge mpinga maendeleo katika
jimbo la Iringa mjini ambalo maendeleo yanaletwa kwa nguvu na ccm"
Bw Mapunda asema
anawashangaa wapinzani kwa kuikataa katibu inayopendekezwa ambayo unazungumzia
pia Haki ya kuishi hivyo kupinga Kwao wanapinga hadi haki ya wao kuishi.
Alisema kuwa hoja Yao
ni kutaka serikali tatu na si vinginevyo na kuwa wananchi lazima wapigie kura
ya ndio katiba hiyo na pindi muda wa serikali tatu utakapofika basi itafanyika
hivyo na si sasa.
Kuwa kuutaka
utanganyika ni kuutaka ukoloni hivyo lazima kujitambua kuwa wakati wa kuongozwa
na wakaloni umepita.
0 comments:
Post a Comment