Monday, July 17, 2017

JUMIA NI CHACHU KWA UKUAJI WA BIASHARA ZA MTANDAONI BARANI AFRIKA

Na Jumia Travel Tanzania

Mwaka 2017 kampuni ya Jumia ambayo inajishughulisha na huduma mbalimbali kwa njia ya mtandao barani Afrika inatimiza miaka mitano tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 2012.

Kampuni hiyo ambapo awali ilikuwa ikijulikana kama Africa Internet Group (AIG) pindi inaanzishwa imejikita zaidi na shughuli zake mtandaoni katika maeneo kama ya huduma za chakula (Jumia Food), manunuzi ya bidhaa mbalimbali (Jumia Market), hoteli na usafiri wa ndege (Jumia Travel), makazi (Jumia House), magari (Jumia Cars), matangazo (Jumia Deals) na kazi (Jumia Jobs).
Katika kuzikabili changamoto zinazolikabili bara la Afrika kama vile miundombinu hafifu kama vile usafiri wa barabara na anga, umbali wa maeneo na foleni ndefu za barabarani ambazo husababisha watu kupoteza muda mwingi kufika maeneo mbalimbali zote hizi zinatoa fursa kwa kutumika njia ya mtandao wa intaneti ili kuokoa muda na gharama.

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA KUABUDU NCHIN


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora  Angela Kairuki akihutubia kwenye mkutano wa kitaifa wa shukrani na kumuombea Rais Dk.John Magufuli pamoja na nchi uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana.

MKUTANO WA KIMATAIFA WA SHUKRANI KUFANYIKA KESHO UWANJA WA UHURU JIJINI DAR ES SALAAM

Muhubiri wa Kimataifa Dk.Nicku Kyungu akihubiri katika kongamano la siku mbili la viongozi wa dini lilifanyika Kanisa la Naoith Pentekoste Church Makuburi jijini Dar es Salaam leo kwa Askofu Dk. David Mwasota. Kongamano hilo linakwenda sanjari na mkutano wa kitaifa wa shukrani wa kuliombea taifa na Rais Dk.John Magufuli utakaofanyika kesho Uwanja wa Uhuru.

Tuesday, July 11, 2017

DED MNASI: WANANCHI WA ILEJE WATANUFAIKA NA ARDHI YAO

 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiwa Na baadhi ya wananchi wa kijiji Shinji
 Mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi akibadilishana mawazo na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Shinji
 
Na fredy Mgunda, Ileje

Wananchi wa Halmashauri ya Ileje Mkoani Songwe kunufaika na maeneneo yaliyotengwa  kwa ajili ya vikundi vya wajasiliamali na Vijana ikiwa ni kuendelea kutekeleza ilani ya chama cha mapindizi chini ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John pombe Magufuli.

Akizungumza wakati wa utowaji elimu na urasimishaji wa maeneo ya vikundi vya vijana vijijini Mkurugenzi wa Halmamashauri hiyo ndugu Haji Mnasi alisema nia ya uongozi wa halimashauri hiyo ni kuhakikisha wananchi wake wananufaika kiuchumi kupitia rasilimali zilizopo katika Wilaya hiyo ikiwemo Ardhi, amesema wananchi wengi wanamiliki Ardhi lakini wanashindwa kuzitumia kupata mikopo kutokana na kutozirasimisha 

Mkurugenzi huyo akiwa pamoja na Watendaji wake (Maafisa Ardhi,Maendeleo ya Jamii na afisa ushirika, wamewatebelea  wananchi vijijini  ili kutoa Elimu ya Uwekezaji na Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi katika Wilaya ya Ileje.

Pia Mnasi alisema Lengo la ziara hiyo akiawa na wataalam wa kada hizo ilikuwa ni Kuhakikisha kuwa halmashauri inawezesha Urasimishaji na Uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi kwa kupitia Vyama vya Ushirika na Vikundi vya kiuchumi na kijamii Vilivyo sajiliwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya. 

Ziara hii ya vijijini imewezesha mambo yafatayo kufanyika:

1. Kubaini maeneo yaliyo tengwa na Vikundi vyenyewe au Serikali ya kijiji kwa ajili ya Shughuli za Vikundi hivyo. 

2. Kurasimisha Maeneo yaliyobainishwa kwa ajili ya shughuli za Kikundi cha Mpozile katika kijiji  cha Msia, Kikundi cha Umoja katika kijiji cha Shinji yamebainishwa, kupimwa na yako katika mchakato wa kutwaa hati miliki ya maeneo hayo na Vijana SACCOS ya Yuli katika kijiji cha Yuli 

Mkurugenzi huyo wa Ileje Mkoani Songwe alisema watahakikisha eanashirikiana na wananchi kwa kwenda vijijini bila kuwasubilia wao kufika ofisini, bali kuwafuata na kutatua changamoto  ili kuendana Na kasi ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania katika kutekeleza Sera ya  chamaa cha mapinduzi CCM.

Afisa ardhi  Daniel Mpagama na afisa maendeleo vijana na uwekezaji David Gunzar walimpongeza Mkurugenzi huyo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo katika wilaya ya Ileje na kuwaomba wafanyakazi wengine kuunga mkono ili kufikia malengo.

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Shinji Daudi Kanyika alisema kuwa hajawahi kumuona Mkurugenzi kama huyo kwa kuwa wakurugenzi wengi huwa wanashinda maofisini tu ila Mkurugenzi Mnasi amefika hadi huku kijijini na kutufungulia fursa za kimaendeleo

NDOA ZA KIHISTORIA KUFUNGWA SIKU MOJA NDANI YA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA

Turn off for: Swahili Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya waliookoka katika kanisa hilo huku tayari wakiwa wanaishi na wenza wao kama mme na mke bila kufunga ndoa takatifu, wamepata fursa ya kufungishwa rasmi ndoa takatifu. Mchungaji wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola amesema si vyema waliookoa kuishi kama mme na mke huku wakiwa hawajafunga ndoa takatifu madhabahuni mwa Bwana hivyo jumapili ijayo Julai 16,2017 zitafungwa ndoa za pamoja zaidi ya tisa kwa waumini waliookoka huku tayari wako kwenye ndoa bubu. "Usikae na mme au mke bila kufunga ndoa, maana ndoa bubu itakukotea puani. Acha kuvaa mapete ya ajabu ajabu bila kufunga ndoa. Unakuta lipete lina kichwa cha nyoka, jiulize hilo lipete umepewa na nani? Huenda ndiyo maana unaandamwa na mapepo". Alisisitiza Dkt.Mchungaji Kulola. Baadhi ya wanaotarajiwa kufunga ndoa siku hiyo, wamefurahishwa na fursa waliyoipata huku wakisema aina hiyo ya ndoa ni nzuri kwa kuwa hawatatumia gharama kubwa kwani baada ya kufunga ndoa, watapata chakula cha pamoja kanisani hapo na baadaye kurejea nyumbani. Tukio hilo la kihistoria litaanza saa nane kamili mchana katika kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Jijini Mwanza na watu wote wanakaribishwa kulishuhudia ambapo baada ya ndoa hizo kufungwa, itafanyika tafrija fupi kanisani hapo ambapo watu watakula na kunywa pamoja na wanandoa hao. [caption id="attachment_27228" align="aligncenter" width="620"] Mwenyekiti wa kamati ya harusi (kushoto) na katibu wake.[/caption]

Amil Shivji aelezea filamu ya T-Junction iliyofungua pazia tamasha la ZIFF 2017

Mwandishi na Muongozaji wa filamu katika kampuni ya KIJIWENI Production, Amil Shivji ambaye yupo visiwani hapa Zanzibar na ‘crew’ yake ameelezea kwa kina filamu yake mpya na ya pili katika filamu makala ijulikanayo kama ‘T-JUNCTION’ ambayo usiku wa Jumamosi wa Julai 8,2017 imepata kuwa filamu ya kipekee huku ikishuhudiwa na Rais Mstaafu wa awami ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa tamasha la filamu la Kimataifa la nchi za Jahazi (ZIFF) ambalo mwaka huu linaadhimisha miaka 20, tokea kuanzishwa kwake. Akizungumza na wanahabari pamoja na wadau wa filamu katika mkutano maalum wa ZIFF, Amil Shivji amebainisha kuwa, T-JUNCTION ni filamu ya pili ya Kijiweni Productions, na amejisikia furaha na thamani kubwa yeye na ‘Crew’ yake kwa mara ya kwanza kuweza kuzinduliwa kidunia kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya tamasha la ZIFF mwaka huu kwani ni fursa ya kipekee katika njia ya mafanikio ya filamu hiyo. Amil Shivji amefafanua kuwa, T-Junction inawatambulisha mabinti wawili katika tasnia la filamu akiwemo; Hawa Ally (Fatima) na Magdalena Christopher (Maria) huku pia ikishirikisha sura mpya, Mariam Rashid (Mama Fatima), Sabrina Kumba (Mama Maria) akiwemo pia David Msia (Chine) katika jamii wa waigizaji. “Mbali na sura hizi mpya katika filamu hii. Pia tumeweza kuchanganya na waigizaji mashuhuri kama Cojack Chilo akiicheza kama Iddi, mkaka mkimya na mwenye imani. Mzome Mohamed (Mangi) na Tin White akicheza kama Shabani mkaka mchangamfu na mcheshi.” Alieleza Amil Shivji. Shivji ameendelea kufafanua kuwa, Kuhusu Filamu hiyo ya T-Junction ni kisa kinachowahusu mabinti wawili na jamii zao. Jamii moja ikiishi kiholela huku faraja yao ni kujua wana umoja na furaha. Jamii yao inazingatia sana mifumo, kanuni na taratibu za utu. Fatima, kigoli mwenye asili ya kihindi na kiafrika amefiwa na baba yake kutokana na pombe. Anashindwa kumuombolezea maana kwa kweli hawakuwa na ukaribu wowote. Hakupata kuwa karibu nae katika uhai wake, waliishi katika giza la utengano. T-Junction ni filamu inayohusu matabaka katika jamii ya Kitanzania. Ambapo jamii ya daraja la chini kabisa wanapambana na misukosuko vinavyowakabili ambapo miongoni mwa mambo hayo na mengine yenye visa vya kukufanya ubaki kinywa wazi na hata wakati mwingine kuangusha chozi ama kucheka kwa kufurahia kwa hali ya juu kwani kila muhusika ameweza kuitendea haki nafasi aliyopangiwa. Kijiweni Production: Amil Shivji anabainisha kuwa, kupitia kampuni yao hiyo, wameweza kuendelea kupata mafanikio makubwa ya kufanya vizuri kwa filamu zake mbili Shoeshine na Samaki Mchangani na filamu ya Aisha iliyokuwa na mafanikio makubwa.
Mwandishi na Muongozaji wa filamu katika kampuni ya KIJIWENI Production, Amil Shivji akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa masuala ya filamu (hawapo pichani) mapema leo Julai 9,2017 wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Hata hivyo, Amil Shivji amewekwa wazi kuwa, kuwa filamu hiyo ya T-junction kutokana na kisa cha kweli kilichotokea eneo la Upanga. Eneo aliloishi tangu kipindi cha utoto wake. Ameendelea kuchunguza ukinzani wa matabaka dhidi ya ukuaji wa maeneo ya mjini kwa kasi. “Filamu hii imenichukua zaidi ya miaka 6, kuanzia kuifikilia na hata kuchukua maamuzi ya kuiandaa na hadi nikatimiza malengo yangu kwani ilikuwa ipo kichwani mwangu tokea utotoni mwangu na nimeweza kufanya kitu” ameeleza Amil Shivji. Shivji ameongeza kuwa, filamu hiyo iliweza kuwakusanya pamoja zaidi ya watu 30 wakiwa ni wenye ujuzi wa sanaa na watu wenye ujuzi tofauti kutoka tasnia ya filamu kwa takribani siku 20, kuanzia mwezi Februari mpaka mwezi Machi mwanzoni huku upigaji picha (shooting) ukifanyika kwenye maeneo tofauti ya Jiji la Dar es salaam. “T-Junction ni filamu ambayo kwa hakika inaonyesha vipaji vilivyopo katika tasnia ya filamu Tanzana. Tunajivunia kwamba baada ya maadhimisho ya kidunia katika tamasha la ZIFF, T-Junction itaonyeshwa kwa mara nyingine katika jijini la Dar se salaam (Tanzania Bara) hasa katika kumbi kubwa za sinema ikiwemo Century Cinemax- Mlimani City mwezi wa Agosti mwaka huu, tunawaomba watanzania na watu wote kuweza kujitokeza kwa wingi kuishuhudia filamu hii kwani imejaa mambo mengi na yenye mafunzo” alimalizia Amil Shivji. Kwa upande wao washiriki wageni katika filamu hiyo kwa nyakati tofauti wameelezea kuwa katika hali ya furaha kipindi chote kwani wamejiskia furaha kwa kutazamwa na watu wengi kupitia tamasha hilo ambapo wanaamini nyota zao zitaendelea kung’aa zaidi na zaidi kadri siku zinavyoenda na wanaamini hilo itafanya vizuri.
Mwandishi na Muongozaji wa filamu katika kampuni ya KIJIWENI Production, Amil Shivji akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa masuala ya filamu mapema leo Julai 9,2017 wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.

Muigizaji mpya Hawa Ally alietumia jina la Fatuma akielezea namna alivyoweza kuucheza uhusika kwenye filamu ya T-junction. Kushoto ni Mwandishi na Muongozaji wa filamu katika kampuni ya KIJIWENI Production, Amil Shivji mapema leo Julai 9,2017 wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.

Mwandishi na Muongozaji wa filamu katika kampuni ya KIJIWENI Production, Amil Shivji akiwatambulisha Hawa Ally (Fatima) na Magdalena Christopher (Maria) mapema leo Julai 9,2017 wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.

Amil Shivji akiwa pamoja na 'Crew' yake pamoja na mgeni rasmi Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete (katikati)

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa KIJIWENI PRODUCTION mara baada ya uzinduzi wa tamasha la ZIFF 2017.

Amil Shivji (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) na Baba yake Mzazi, Profesa Issa Shivji mara baada ya uzinduzi huo wa tamasha la 20 la ZIFF 2017. (PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE).

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI JUNI,2017 WAPUNGUA KWA ASIMILIA 5.4

 Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigwabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leokuhusu mfumuko wa bei wa Taifa kwa Mwezi Juni. Kulia  ni Meneja wa Takwimu za Bei na Ajira, Ruth Minja.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwezi Juni  umepungua hadi kufikia asilimia 5.4 ikilinganishwa na asilimia 6.1 ilivyokuwa mwezi Mei 2017.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa na wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana kuhusu mfumuko huo wa bei.

Kwasigabo alisema kasi hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2017 imepungua zaidi ikilinganishwa na kasi iliyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2017.

"Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 109.10 mwezi Juni,2017 kutoka 103.47 mwezi Juni 2016" alisema Kwesigabo.

Alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Juni 2017 umepungua hadi hadi asilimia 9.6 kutoka asilimia 11.6 ilivyokuwa mwezi Mei,2017

Alisema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka kwa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Juni 2017 umepungua hadi kufikia asilimia 9.8 kutoka asilimia 11.8 mwezi Mei 2017.

Aliongeza kuwa badiliko la fahirisi za bei kwa bidhaa zisizo za vyakula umeongezeka hadi asilimia 3.11 mwezi Juni 2017 kutoka asilimia 3.1 mwezi Juni, 2017 kutoka asilimia 3.0 mwezi Mei 2017.

Monday, July 3, 2017

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUTUMIA HUDUMA ZA HOTELI MTANDAONI


Na Jumia Travel Tanzania

Kuna faida nyingi za kutumia mitandao inayotoa huduma za hoteli badala ya kuwasiliana nao au kutembelea tovuti zao moja kwa moja. Kwani unaweza kuperuzi aina tofauti za hoteli, kujua huduma walizonazo pamoja na bei kabla ya kufanya maamuzi ni hoteli gani umependezewa nayo.

Mbali na kuwepo kwa manufaa mengi kwa mteja pindi anafanya huduma za hoteli mtandaoni changamoto kubwa hujitokeza kwenye kufanya uchaguzi na maamuzi. Jumia Travel ingependa kukushirika mambo muhimu ya kuzingatia pindi unapoingia mtandaoni na kuchagua ni hoteli gani unayotaka kwenda.

Wapi unaweza kufanyia huduma hizo? Kwa wasafiri wengi wazoefu wanafahamu kuwa ni gharama kubwa kutumia huduma za hoteli kupitia kwenye tovuti zao. Badala yake hutumia mitandao inayotoa huduma hizo kwani huwa na bei nafuu tena na ofa kadha wa kadha. Kwa mfano, mmojawapo ya mitandao hiyo ni pamoja na Jumia Travel, ambao una aina mbalimbali za huduma za malazi kwa watu wa hadhi tofauti. Tofauti ya mitando hii na tovuti za hoteli ni kwamba zenyewe zinampatia mteja machaguo ya hoteli mbalimbali, mahali popote na kwa mujibu wa bajeti aliyonayo.
 
Fikiria kuhusu umbali, kufikika kwake na gharama za usafiri. Jambo linalofuatia baada ya kujua ni mtandao gani unaoweza kuutumia kupata huduma unayoitaka ni mahali unapotaka kwenda. Lakini pia ni vema kujiuliza je hapo unapotaka kwenda kunafikika kiurahisi na gharama za usafiri zikoje kukutoa kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Usipokuwa makini unaweza kujikuta unakwenda kufikia sehemu ambayo itakupasa kutumia gharama kubwa za usafiri au ni ngumu kufika kwenda kwenye shughuli zako.

Chumba cha aina gani unachokipendelea? Hoteli au sehemu yoyote ile ya malazi inakuwa na machaguo tofauti kulingana na matakwa ya mteja. Kuna huduma ya chumba kimoja, chumba kimoja chenye vitanda viwili ndani, chumba chenye maliwato ndani yake na kadhalika. Hivyo lazima ujue ni chumba cha aina gani unakitaka ili hata iwe rahisi kumuelezea mtoa huduma hotelini, lakini hayo yote hutegemea bajeti yako kwani bei huwa tofauti.

Je unaweza kupata huduma siku hiyo hiyo? Dharura hutokea na huwa haiepukiki kwenye masuala ya kusafiri. Kwa mfano unaweza kupewa maagizo na bosi wako kusafiri kwenda mkoani siku hiyo hiyo na tayari tiketi ya usafiri umekwishakatiwa. Sio hoteli zote zinakubali au kupokea huduma kwa siku hiyo hiyo, hivyo yakupasa kutafiti ni hoteli gani zinafanya hivyo.



Pitia maoni ya wateja waliowahi kukaa hapo. Kuna umuhimu wa kutafiti wateja waliowahi kukaa sehemu unayotaka kwenda wanasemaje kuhusu huduma zao. Hii itakusaidia kujua kwamba itakufaa au la. Sidhani kama utashawishika kwenda kwenye hoteli ambayo wateja wameacha maoni mtandaoni kwamba wahudumu wa pale sio rafiki na wala hakuna ulinzi wa kutosha.

Wateja wanaopendelea sehemu hiyo ni watu wa aina gani? Hoteli huwa zinajengwa kwa malengo tofauti kulingana na aina fulani ya wateja. Zipo kwa ajili ya wafanyabiashara, familia, fungate kwa wanandoa, watalii na kadhalika. Kama wewe ni mfanyabiashara basi chagua hoteli itakayokufaa kwa dhumuni ulilonalo, usije kujikuta unakwenda kwenye hoteli ambayo wanafamilia na watoto huwa wanapenda kwenda kupumzika na ukakwazika.

Huduma nyinginezo - maegesho ya magari, kifungua kinywa, bwawa la kuogelea, sehemu ya kufanyia mazoezi. Kama msafiri na mara nyingi huwa sio wenyeji kwa mahali unapokwenda ni vema kujua ni huduma gani unaweza kuzipata kwenye hoteli unayotaka kwenda. Mfano wa huduma nyingi zinazotolewa na hoteli kwa sasa ni kama vile, kifungua kinywa, maegesho ya magari, mgahawa au chakula, kufuliwa na kupasiwa nguo na huduma ya usafiri. Kwa hiyo pindi unapoamua unakwenda kufikia wapi ulizia vitu hivyo ili kujua kama vinapatikana bure au kuna gharama utakazoziingia kama mteja.





Namna ya kufanya malipo. Sio hoteli zote zinaruhusu kufanya malipo taslimu pale unapofika hotelini na sio zote pia huruhusu mteja kutumia benki au mtandao. Kwa hiyo itakuwa ni jambo la msingi kujua sera ya malipo ya hoteli unayotaka kwenda. Kwani unaweza kukuta kuna hoteli nyingine inakupasa kulipia siku 2 kabla ya kwenda pale au hata wiki moja nyuma. Mara nyingi hii hufanyika ili kuzuia tabia ya wateja kusema wanakwenda halafu hubadili maamuzi, hoteli huwatoza kiasi kadhaa cha fedha wateja wenye tabia hizi ili kuepuka hasara.

Muda wa kuingia na kutoka. Kwa sababu umekwishalipia huduma kwenye hoteli fulani haimaanishi kwamba unaweza kwenda au kutoka muda wowote unaoutaka wewe. Kila hoteli inakuwa na utaratibu wake iliyojiwekee na ni muhimu kuzingatia kwani unaweza kujuikuta unakosa huduma uliyokwishailipia au kuingia matatizoni. Kwa mfano, sehemu nyingi za malazi hapa Tanzania muda wa wateja kuingia hotelini huwa ni saa 4 au 5 asubuhi na kutoka pia inakuwa ni hivyo hivyo siku inayofuatia.
 
Kwa dondoo hizo chache Jumia Travel inaamini kuwa utakuwa umepata mambo mapya ya kujifunza na wakati mwingine utakuwa makini kama ulikosea kipindi cha nyuma. Kufanya huduma za hoteli kwa njia ya mtandao ni kitu ambacho kinatumika duniani kote kwa sasa kwani ni njia rahisi, uhakika na salama. Kikubwa ni kuweza kujifunza namna ya kufanya hivyo kwani kuna faida lukuki badala ya kutumia njia za kawaida tulizozioea kama vile kuwapigia simu ndugu, jamaa na marafiki zako wakusaidie kufanya hivyo huko uendako.

DC MUFINDI: VIJANA MNAOFUZU MAFUNZO YA JKT MUWE WALINZI NAMBA MOJA WA NCHI YENU.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William, akikagua gwalide la vijana wa JKT kama mgeni wa Heshima.
 Vijana wa JKT wanaohitimu mafunzo ya awali, wakipita mbele ya Mgeni wa heshima kutoa heshima ya kijeshi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Profesa. Riziki Shemdoe, akipokea heshima ya kijeshi Mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za kambi ya 841 Mafinga kushiriki maafali hayo.

Na Ofisa Habari Mufindi

Serikali Wilayani Mufindi, amewataka vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya kujitolea ya Jeshi la kujenga Taifa JKT kikosi cha 841 Mafinga, kuwa walinzi namba moja wa amani katika jamii zao, kwa kuwafichua waharifu watakao jaribu kuhatarisha amani na utulivu uliopo nchini kwa sasa

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh. Jamhuri William, wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa vijana waliokuwa wakihudhuria mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa kutoka kikosi cha 841 kilichopo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi.

 “ kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na maadui wa nje na ndani ya nchi wanaojaribu kuvunja Amani na utulivu uliostawi kwa muda mrefu hapa nchini, hivyo, nawaagiza  Mkalinde  kiapo chenu cha utii na uadilifu kwa Taifa na Mkuu wa nchi kwa kutekeleza sera ya Taifa inayotanabaisha kuwa  kila raia wa Tanzania ni Mlinzi wa nchi yake”

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewaasa vijana watakao pata fursa ya kuajiriwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama mara baada ya kuhitimu mafunzo, wakafanye kazi kwa nidhamu, uadilifu na uaminifu na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuajiri vijana wa JKT pekee kwenye sekta zote zinazohusika na ulinzi na usalama wa nchi.

Jumla ya vijana (846) wavulana wakiwa (612 ) na wasichana (234) wenye elimu za Msingi mpaka chuo kikuu, wamehitumu mafunzo ya awali ya kijeshi ya miezi (06) na kufuzu kuingia hatua ya pili ya mafunzo ya Malezi na stadi za kazi katika Jeshi la kujenga Taifa JKT.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More