Friday, July 24, 2015

Kibiki aikumbuka Lipuli, asema ni agenda yake akipata Ubunge



NA MWANDISHI WETU, IRINGA

MGOMBEA wa nafasi ya Ubunge kwa tiketi ya CCM, Mwanahabari Frank Kibiki ameahidi kushirikiana na wadau wa soka kupandisha daraja timu ya soka ya Lipuli ya mjini Iringa iwapo atapewa ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza wakati wa kampeni za kujinadi zilizofanyika katika eneo la Kihesa kilolo, mjini Iringa Kibiki alisema michezo ni fursa ambayo inaweza kuinua uchumi wa mkoa wa Iringa endapo itapatiwa kipaumbele.

Alisema ikiwa atapewa ridhaa ya kuwa mbunge, atakaa chini na wadau wa soka wa manispaa ya Iringa na kuweka mikakati madhubuti ili kuhakikisha wananchi Lipuli inapanda daraja.

“Ndugu zangu, Lipuli ikipanda daraja uchumi wa Iringa mjini utakuwa kwa sababu vijana watapata ajira kwa sababu kwenye uwanja wetu wa samora, zitachezwa timu za kimataifa,” alisema Kibiki.

Aidha alisema kuwa ataimarisha timu nyingine za mjini Iringa ili ziweze kupanda madaraja sambamba na kuinua sekta ya sanaa hasa muziki.

Katika hatua nyingine, Kibiki aliwashauri vijana  kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali na kutumia  fursa zilizopo kwenye  maeneo yao ili waweze kujiajiri na hivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha.

Kibiki alisema, umoja ni nguvu na ikiwa vijana watajiunga kwenye vikundi hivyo vya kiujasiriamali itakuwa rahisi kufanikiwa kiuchumi.

Alisema maeneo mengi ambayo vijana wameungana wameweza kukopeshwa, na wanaendesha shughuli zao za kiuchumi bila wasi wasi, jambo hilo linawezekana.
Mwisho.

Friday, July 17, 2015

MBUNGE WA JIMBO LA ISMANI WILIAMU LUKUVI APATA WAPINZANI JIMBONI KWAKE


mtia nia wa ccm jimbo la ismani festo kiswaga akiwa katika ofisi za ccm jimbo la iringa vijiji
akiwa na katibu wa ccm iringa vijijini

NA MWANDISHI WETU,IRINGA.

Baada ya zoezi la uchaguzi wa wagombea urais kukamilika katika vyama sasa zoezi limeanza kwa wabunge na madiwani ambapo hii leo Festo Kiswaga ambaye ameweka nia ya kugombea katika jimbo la isiman.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari KIswaga amekanusha uvumi uliokuwa umezagaa juu ya kuhongwa pesa mwaka 2010 ili kutogombea huku akidai kuwa alishindwa kwa haiki na si hongo ya mbunge aliyepo madalakani kwasasa huku akimzawadia ukuu wa wilaya.

Ambapo pia ametumia mkutano huo ili kuujulisha uma juu ya maelengo yake ya kuchukua form katika wasifu wake amesema anadigree ya sayansi ya wanyama poli na kutumikia katika shirika la mbomipa na kuwatumikia wananchi wa misenyi mkoa wa kagera akiwa ni mkuu wa wilaya na sasa ni mkuu wa wilaya ya Nanyumbu huku akitumikia mashirika kama tanapa na chuo kikuu cha dar es-laam na kuteuliwa kuwa rais wa wa shirikisho vyuo vikuu vya umoja wa Afrika mashariki uliojumuisha vyou vikuu zaidi ya  400 katika nchi za Tanzania,Uganda,Kenya na Burundi.

Akizungumzia kuhusu janga la njaa lililopo katika jimbo hilo amekiri kuwa anauzoefu juu ya utatuzi wa matatizo kama hayo kutokana na nyanja mbalimbali ambazo amepitia na pia amewataka wananchi wa ismani kumpa lidhaa yya kuwaongoza kutokana tatizo kama hilo amelikuta katika wilaya ya Namnyumbu na akafanikiwa kulitatua kwa asilimia 100%.

Aidha amesema kutokana na jimbo hilo kukosa kiongozi mwenye uchungu kama yeye imepelekea kukosekana kwa huduma kama maji katika vijiji mbalimbali ikiwa jimbo hilo limefikisha miaka 20 ikiwa mashirika mbalimbali na serikali licha ya kuchangia lakini ukosefu wa maji umekuwa tatizo si kwa binadamu tuu bali hata kwa mifugo ambapo hupelekea wananchi kununua maji hadi kwa shiringi mia 500.

Kwaupande wa wananchi waliohudhulia mkutano huo wamekiri kuwapo kwa tatizo hilo ambalo imekuwapo kwa miaka mingi sasa hali inyopelekea wananchi upeleka mifugo yao kunywesha usiku wa manane hali ambayo ineza kuhatarisha usalama wa mifugo hiyo.



Nao kinamama wamekiri kuwa tatizo hilo limekuwa likiwaathiri kiuchumi kwakuwa hutumia muda mwingi katika kutafuta maji bila kufanya shughuli nyingine kwaajiri ya kujenga uchumi wao na wanchi.


Monday, July 13, 2015

MWENYEKITI WA BAVICHA AMVAA MCHUNGAJI MSIGWA UBUNGE IRINGA MJINI


na fredy mgunda,iringa


MWENYEKITI wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), Leonce Marto amechukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Iringa kupitia chama chake hicho.

Amechukua fomu hiyo siku moja tu baada ya Rais Jakaya Kikwete kulihutubia na hatimaye kulivunja bunge la 10 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo uhai wake utakoma Agosti 20, mwaka huu.

Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, jimbo la Iringa Mjini limekuwa likiongozwa na Mchungaji Peter Msigwa ambaye pia alichaguliwa kupitia Chadema katika uchaguzi wa 2010.

Kwa kupitia taarifa yake aliyoisambaza kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii jana, Marto alisema;  “nawasalimu nyote wenye mapenzi mema na Taifa letu la Tanzania na wapenda mabadiliko na demokrasia za ushindani ndani ya vyama vya siasa kwa minajili ya katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 .”

 “Nianze kwa kuwashukuru watu wote  ambao kwa muda wa uhai wangu wameshiriki kwa namna moja ama nyingine kuniwezesha  kufika hapa nilipo . Pili nawashukuru viongozi , wanachama , wafuasi wa Chadema, ndugu,  jamaa na marafiki ambao kwa wingi wenu sitaweza kuwataja wote,” alisema.

Marto alisema ameamua kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mchungaji Msigwa baada ya kupata msukumo wa ndani na nje ya chama.

Alisema kwa haraka katika fahamu zake aliona jambo hilo ni zito na la hatari kulinganisha na watu wanavyosema kwasababu kazi ya umma ni kazi inayohitaji dhamira safi, uadilifu, umahiri, weledi, kujali ya maisha ya watu na maendeleo yao na zaidi sana kupenda na kutathmini Taifa na watu wake.

Marto alisema ilimchukua muda kujiridhisha pasipo shaka na jambo hilo kama  anaweza kubeba wito huo wa kuwatumikia wananchi wa Iringa Mjini.

“Baada ya kutafakari kwa kina nilijipa mtihani wa kwanza wa kuzunguka nchi yetu na kukutana na jamii za watanzania. Kwa mantiki hiyo ninayafahamu kwa undani na kwa uhalisia wake maswala na matatizo muhimu yanayowakabili watanzania na wana Iringa Mjini,”alisema.

Marto alisema kwa kuwa anakidhi vigezo vya kikatiba, na kwa kuwa anaamini Mungu amempa karama ya uongozi ambayo watu wameiona na kumuomba agombee ubunge na kwa kuwa anayajua matatizo yanayowakabili watanzania na wana Iringa anayajua na yamemchosha kama yalivyowachosha watanzania wengine:


Na kwa kuwa Chadema kimejengwa kwenye mhimili na msingi mkuu wa Demokrasia pamoja na itikadi na falsafa yake ya Nguvu ya Umma na kwa kuwa anaamini viongozi bora wanapatikana kwa ushindani, kwa ujasiri wote aliopewa na Mwenyezi Mungu anatangaza rasmi kuomba ridhaa ya chama chake kugombea ubunge katika jimbo hilo.

Wednesday, July 8, 2015

Mamia ya wana Iringa waendelea kumchangia Mwanahabari Kibiki achukue fomu ya Ubunge Iringa mjini






 
na fredy mgunda,iringa
 WAKATI joto la uchaguzi likiendelea kupanda katika jimbo la Iringa mjini, mamia ya vijana, wanawake, walemavu  na wazee katika jimbo hilo wanaendelea kuchangishana fedha ili kumuwezesha mwanahabari Frank Kibiki kuchukua fomu ya kuomba ateuliwe kupeperusha bendera ya CCM, kwenye jimbo hilo.
Zoezi hilo linaloendeshwa na baadhi ya vijana waliomtaka Kibiki ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM taifa, kutotoa rushwa badala yake atumie hoja kuelezea sera zake, walisema wameamua kuchangishana fedha ili kumuwezesha kijana huyo kuchukua fomu.
Wakizungumza na wanahabari, tayari vijana hao walisha mkabidhi Kibiki zaidi ya Sh 200,000 miezi mitatu iliyopita.
“Bei ya fomu ni 100,000 pamoja na michango inafikia 500,000 kwa kuwa tunahitaji kijana kutoka miongoni mwetu, tumeamua kumuwezesha Kibiki ili atuwakilishe kwenye jimbo letu kupitia CCM, hatutaki atoe rushwa kununua uongozi, kwa sababu sisi ndio tunamuajiri kuwa mtumishi wetu,” alisema Salum Mwinami, kada wa CCM.
Michango hiyo inaendelea katika maeneo ya stendi kuu ya mabasi, stendi ya daladala ya miyomboni, Kihesa, Mtwivila, Kitwiru, Ipogoro na chuo kikuu cha Iringa.
Tangu Kibiki atangaze nia ya kuwania jimbo la Irnga mjini, hali ya upepo wa jimbo hilo imebadilika huku wananchi wakiitaka CCM itende haki badala ya kuwakumbatia wanaotumia rushwa, kutaka madaraka.
Mpaka sasa wanachama wa CCM wanaotajwa kuomba ridhaa ya CCM kuwania jimbo hilo wanafikia 10, akiwemo Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Iringa, Jesca Msmbatavangu na Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM ya jimbo hilo, Mahamud Madenge.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Kibiki aliwashukuru wananchi wanaomchangia fedha hizo ili achukue fomu na kuahidi kuwa atafuata kanuni na taratibu za chama hicho ili asikose sifa za kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM kwenye jimbo hilo ikiwa atashinda.
“Nawashukuru sana wana Iringa mnaonichangia fedha ili kuniwezesha kuchukua fomu, nathamini utu wenu nachowaomba mniombee,” alisema.

Monday, July 6, 2015

WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA IRINGA CHAMPONGEZA ELISHA MWAMPASHI KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA KATIKA JIMBO LA IRINGA MJINI



katibu wa jimbo la iringa mjini ELISHA MWAMPASHI
katibu wa jimbo la iringa mjini ELISHA MWAMPASHI
 KEKI ILIYOKUWA IMEANDALIWA SIKU YA SHEREHE HIYO.
 Baadhi  ya wanachama wa chama cha mapinduzi tawi la chuo kikuu cha iringa zamani tumaini.

 NA FREDY MGUNDA,IRINGA

Baadhi  ya wanachama wa chama cha mapinduzi tawi la chuo kikuu cha iringa zamani tumaini wamefanya maafari yao katika ukumbi wa chama hicho sabasaba.

Wakizungumza wakati wa sherehe hiyo wanafunzi hao wamesema kuwa sas ccm italajia kurudisha jimbo la iringa mjini kwasababu tayari makatibu wa chama hicho wameweza kuwarudisha vijana kukipenda chama hicho.

Aidha wamesema kuwa  chama hicho kilipoteza mvuto kwa vijana na vijana walipoteza mvuto na chama hicho,hivyo chama hicho kwa sasa kimerudisha  imani kwa vijana na wanachama wengine.

“Sisi hapa chuoni kwetu tulikuwa wanachama  wachache ila kwa sasa tupo wengi na kila siku wanachama wanazidi kuongezeka kutokana na kukipenda cha hicho kwa wakati huu tukielekea katika uchaguzi mkuu”walisema wanafunzi hao.

Mbunge wa jimbo hili kwa sasa mchungaji PETTER MSIGWA ajiandae kuondoka kutoka na chama hicho kujipanga kila kona na tayari wamejihakikishia ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kuongeza kuwa wananchi wa manispaa ya iringa wanapenda amani na sio vurugu.

Lakini walimpongeza katibu wa jimbo la iringa mjini ELISHA MWAMPASHI kwa kufanya kazi  nzuri iliyosababisha wananchi wa jimbo hili kurudisha imani na chama hichi na kuongeza kuwa MWAMPASHI ni kiongozi mzuri na anajua majukumu yake hivyo ni vizuri wananchi wa manispaa tukashikiana na jembe hili kulikomboa jimbo hili.

Kwa upande wake KATIBU WA JIMBO HILI ELISHA MWAMPASHE ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo aliwapongeza wanachama wa chama hicho tawi la tumaini kwa kukikuza chama hicho na kuongeza wanachama.

MWAMPASHI akawataka wanachama hao kukipigania chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao ili waweze kushinda kwa kishindo kikubwa na kuwaachawapinzani hoi.

“Tunanguvu na nia ya kufanya vizuri katika uchaguzi wa mwaka huu kwa kuwa tumejipanga kili kona na tumerudisha inmani kwa wananchi wote hivyo kazi kwa sasa imekuwa rahisi hasa kulikomboa jimbo la iringa mjini ambalo walilikopesha kwa mpinzani”alisema MWAMPASHI.

Aidha MWAMPASHI aliwataka wananfunzi kuacha kufanya mambo ya kizinaa pindi wapatapo kazi kwa kudai kuwa anakura ujana ,akaongeza kuwa sasa ni wakati wa vijana kuwekeza katika biashara mbalimbali ili kujitengenezea maisha mazuri hapo baadae.

“Nawaomba jamani tusiwe na tamaa katika kutafuta maendeleo kwa kuiba au kutoa na kupokea rushwa  kwa kuwa hiyo njia sia sahihi kwani hapo mtakuwa mkirudisha maendeleo nyuma na sio kuendelea kuleta maendeleo”.alisema MWAMPASHI.

Alimalizia kwa kumtaka mbuge wa jimbo hili kufungasha vitu vyake kwa kuwa muda wake umeisha na wananchi wa manispaa ya iringa wamemchoka kwa kuwa toka ameingia madarakani hakuna alichokifanya katka kuleta maendeleo ya jimbo hili zaidi kuanzisha migomo na vurugu katika sehemu mbalimbali.


Friday, July 3, 2015

CHUO KIKUU CHA IRINGA ZAMANI TUMAINI KESHO KINATARAJIA KUADHIMISHA SIKU YA UTALII NA UTAMADUNI MAADHIMISHO YATAFANYIKA KATIKA CHUO HICHO.

 
 MHADHILI WA CHUO KIKUU CHA IRINGA JIMSON SANGA 
 
 baadhi ya majengo ya chuo kikuu cha iringa zamani tumaini
 
  baadhi ya majengo ya chuo kikuu cha iringa zamani tumaini

na fredy mgunda,iringa



Chuo kikuu cha IRINGA ZAMANI TUMAINI kesho kinatarajiwa kuadhimisha siku ya utalii wa kitamaduni  katika chuo hicho.


Akizungumza na blog hii mkuu wa kitengo cha utalii cha chuo  hicho MHADHILI WA CHUO KIKUU CHA IRINGA JIMSON SANGA amesema kuwa wameamua kuadhimisha siku hiyo ili kuwakumbusha wananchi juu ya kuuezi utamaduni wao na kuacha kuiga tamaduni za kigeni.


Aidha SANGA amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikifundisha elimu ya utalii ndani ya chuo tu sasa imefika wakati wa kutoka na kuifikia moja kwa moja  jamii ambayo haina elimu hiyo.


“Tunaona wakina mama ntilie wanauza vyakula ya kitamaduni lakini hawana wateja kwa sababu wanashindwa kutoa huduma ya kuridhisha kwa wateja hata hivyo mama ntilie wengine hutoa huduma kwa kutofata mazingira ya kiafya”.alisema SANGA


Ameongeza kuwa watanzania  wengi hatuna tabia ya kuupenda utamaduni wetu au kuipenda asili yetu tunaona wananchi wengi wanapenda kuiga utamaduni wa kigeni hivyo tunatakiwa kuuenzi utamaduni wetu.


SANGA amemalizia kwa kuwataka wanachi wajitokeze siku ya jumamosi ili kujionea vitu mbalimbali ya kitamaduni.


Kwa upande wao WANAFUNZI WA CHUO HICHO hasa wanaosomea masomo ya maliasili na utalii wamewataka wananchi wa mkoa wa iringa kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hao.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More