frank kibiki akiongea na wananchi stand kuu ya mabas iringa
wananchi wakimsikiza frank kibiki alipokuwa maeneo ya stand kuu
na fredy mgunda,iringa
MATOKEO ya utafiti uliofanywa na taasisi ya Southern Highland Zone
Election Research (SHZER), katika jimbo la Iringa mjini umeonyesha kuwa nyota ya
Mwanahabari , Frank Kibiki aliyetangaza
nia kuwania Ubunge jimbo la Iringa mjini (CCM) inazidi kung’ara baada ya kuongoza
huku akichuana vikali na Mbunge wa sasa Mchungaji Peter Msigwa(CDM).
Utafiti huo uliofanywa kwa miezi minne tangu, kuwepo kwa
wimbi la watu wengi kutangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Iringa
mjini, wakiwemo makada lukuki wa CCM unaonyesha kuwa Nyota ya Frank Kibiki
inazidi kung’ara kutokana na kuungwa mkono na makundi mengi ya kijamii hasa
vijana, wanawake, walemavu na wazee.
Akizungumza na mtandao huu, Mtafiti mkuu wa SHZER, Patson William alisema utafiti huo umefanywa
katika kata 14 za jimbo la Iringa mjini huku wagombea vijana wakiwa ndio wanaoongoza
kupendwa ikilinganishwa na wagombea wenye umri kuanzia miaka 50 na kuendelea.
Kibiki anaongoza kwa asilimia 40.7, Mchungaji Msigwa 20.9,
Jesca Msambatavangu 11.7, Dr Yahaya Msigwa 7.6, Fredrick Mwakalebela 2.8, John Kiteve
2.4, Mahamoud Madenge 1.2 na wengine waliobaki wanagawana asilimia 12.7.
Utafiti huo unaonyesha kuwa, kinachomfanya Kibiki kuendelea
kung’ara ni siasa zake za kistaarabu, taaluma ya uana habari, uwezo mkubwa wa
kujenga na kujibu hoja anazokumbana nazo sambamba na uzoefu katika utendaji
wake wakati akiwa Katibu wa UVCCM katika wilaya mbalimbali alizowahi kufanya
kazi.
Alisema utafiti huo umefanywa kwa njia ya madodoso ambapo
watu 400 walijibu na maswali ya papo kwa papo ambapo watu 1000 waliyajibu.
Alitaja kata zilizohusishwa kuwa ni Makorongoni,
Miyomboni/kitanzini, Kihesa, Kwakilosa, Mlandege, Mivingeni, Gangilonga,
Kitwiru, Igumbilo, Nduli, Ruaha, Mkwawa, Mtwivila na Isakalilo.
Mambo ya msingi ambayo utafiti huo uliangalia ili kutafuta
majibu ni Changamoto za jimbo la Iringa mjini kwa sasa,sifa za Mbunge
anayetakiwa kukabiliana na changamoto hizo, mapendekezo ya jina la atakayesimamia
vizuri changamoto hizo na mazingira ya siasa za sasa za jimbo la Iringa mjini.
Hata hivyo CCM na Chadema ndiyo vyama pekee vinavyochuana
kwa kasi katika jimbo la Iringa mjini, tangu CDM iliponyakua jimbo hilo mwaka
2010.
Hata hivyo utafiti huo unaonyesha kuwa CCM itakuwa na
wakati mgumu ikiwa watateua jina la mtu asiyechaguo la wananchi jambo ambalo,
litampa Mchungaji Msigwa ushindi usio na jasho.
“Utafiti huu unaonyesha kuwa CCM inanafasi nzuri ya
kuchukua jimbo la Iringa mjini ikiwa tu watafuata nini wana Iringa wanasema
vinginevyo, nafasi ya Msigwa kuendelea itakuwa kubwa,”anasema
0 comments:
Post a Comment