Tuesday, May 26, 2015

katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa Elisha Mwampashi awataka vijana kujituma kuafanya kazi na kuacha kukaa vijiweni


 katibu  wa  UVCCM mkoa  wa  Iringa Elisha Mwampashi wa  pili  kulia akiwa na katibu  mkuu  wa UVCCM Taifa Bw  Sixtus Mapunda

 na fredy mgunda,iringa

Akizungumza na mtandao huu katibu wa uvccm mkoa wa iringa ELISHA MWAMPASHE alisema kuwa vijana wengi wamekuwa wakibweteka kwa kutojituma kufanya kazi na kuendelea kuilaumu serikali.

“Eti asubuhi unawakuta vijana wamekaa kwenye vijiwe wakizungumza siasa na kucheza mabao wakati hawajui mchana watakula wapi na jioni watarudi na nini nyumbani”alisema  ELISHA MWAMPASHE

ELISHA MWAMPASHE ameendelea kuwaomba vijana wengi wenye fursa ya kurudi au kuingia shuleni upya warudi kwa kuwa dunia ya sasa inataka wasomi wengi kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na sayansi na teknolojia na ndio sababu inayopelekea hata watu wazima kurudi shuleni.

“Vijana mnatakiwakujifunza kutoka kwa watu wazima ambavyo wamekuwa wakijituma kufanya kazi kwa bidii na kujituma ilimradi kuwatengenezea watoto maisha mazuri pamoja na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla”alisema  ELISHA MWAMPASHE

Lakini ELISHA MWAMPASHE amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.

ELISHA MWAMPASHE  ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na ushindani wa wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo yasiyokuwepo.

Ameendelea kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.

Aidha ameongeza kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga kura wao hali itakayowafanya waaminike katika jamii.

Mbali na hayo ELISHA MWAMPASHE amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana na sera za chama chake.

Ameendelea kusema kuwa vijana wajitokeze kwa wingi katika kupiga kura ndiyo katika katiba iliyopendekezwa ili kuweza kufanya uchaguzi ulio wa haki na amani pia kujitokeza katika kujiandikisha katika daftari la wapiga kura pamoja na kupiga kura.

Aidha ELISHA MWAMPASHE amewataka vijana wa Manispaa ya Iringa, wametakiwa kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali na kutumia fursa zilizopo kwenye maeneo yao ili waweze kujiajiri na hivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha.


“Tukiungana pamoja ni rahisi kufanikiwa kiuchumi, hakuna njia njia nyingine kwa sababu dhamana yetu vijana ni umoja tu, jiungeni kwenye vikundi vya ujasiriamali,”alisema ELISHA MWAMPASHE


Alisema maeneo mengi ambayo vijana wameungana wameweza kukopeshwa, na wanaendesha shughuli zao za kiuchumi bila wasi wasi, jambo hilo linawezekana.
 

Alisema mpaka sasa wanayo zaidi ya Sh Milioni 10, ambazo wamekuwa wakikopeshana kwa riba naafuu.
Alifafanua kuwa mara nyingi vijana wa stendi wamekuwa wakiachwa nyuma kwenye shughuli za kimaendeleo jambo ambalo, limewafanya waungane.

Monday, May 25, 2015

KUMEKUCHA JIMBO LA ISMANI LUKUVI APATA MPINZANI

 
 WILLIAM LUKUVI MBUNGE WA JIMBO LA ISMANI
 
WILLIAM LUKUVI MBUNGE WA JIMBO LA ISMANI

NA RAYMONDI MINJA IRINGA

MSOMI  wa Digri ya uhandisi wa kilomo na mtaalamu  wa kilimo cha
umwagiliaji kutoka chuo kikuu cha kilimo Sokoine (SUA)Mhandisi
Sebastiani Kayoyo (39) anetangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika
jimbo la Isimani kwa tiketi ya CCM  linaloshikiliwa na Waziri wa
aridhi ,nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi

Akitangaza nia yake hiyo mkoani Iringa juzi  Kayoyo alisema kujitosa
katika jimbo hilo ni kuhakikisha maendeleo yakiongezeka kwa kasi na
kutoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wa jimbo hilo.

Kayoyo alisema kuwa siko kwamba mbunge aliyeko madarakani  hajafanya
mambo ya msingi ila mbunge huyo ameongoza jimbo hilo kwa miaka mingi
hivyo ni fursa ya hazina kubwa ya vijana walioko ndani ya chama cha
mapinduzi kuweza kushika hatamu katika kusukuma mbele  gurudumu la
maendeleo katika nchii hiii

"Mbunge anayeshikiria jimbo ninamheshimu sana na  ameweza kufanya
mambo mengi mazuri, hivyo kwa kidemokrasia nina kuwa na Haki ya msingi
kikatiba, nitahakikisha naendeleza mambo ya msingi ambayo bado
hajayatekeleza, hii ni pamoja na kuongeza nguvu kwa wananchi wengi
waliokosa fursa mbalimbali" kayoyo

Kakoyo ambaye kwa sasa ni mwajiriwa wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Rukwa
kama muhandisi wa kilimo (Mtaalamu wa zana za kilimoba kilimo cha
umwagiliaji )ni mzaliwa wa kijiji cha Tungamalenda kata ya idodi
tarafa uya idodi  iliyopo ndani ya Jimbo hilo la Isimani

Alipoulizwa kuhusiana na hatima ya ajira yake endapo ataukosa ubunge
,”Mimi ni mtumishi wa serekalina ninajua raratibu zote za utumishi
serekali lakini niko tayari kuacha kazi ili kufanyakazi na ndugu zangu
wa Isimani katika kujiletea maendeleo”

 Akitaja vipaumbele vyake endapo chama chake kitampa ridha ya
kukimbiza kijiti hicho Kayoyo alisema kuwa ataweka msisitizo katika
swala la afya , kilimo ,maji safi na salama pamoja na swala la
miundombinu ikiwemo Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha  lami kwa kwa
kuwa  jimbo hilo halijawahi kuwa na lami tangu nchii hii ilipopata
uhuru wake

"Nia yangu ni kuona maendeleo ya jimbo hilo yakiongezeka, napenda
kuona  wananchi ambao asilimia kubwa ni wakulima wakipata fursa za
kusafirisha mazao yao nje ya jimbo hilo huku vijana nao wakipata
kuwezeshwa, uongozi ni kupokezana kijiti hivyo kijiti hicho
nitakiongoza vizuri na naomba wananchi siku itakapofika ni kutekeleza
wajibu" alisema Kayoyo

Kwa kujitokeza huko kwa Kayoyo  kunafanya idadi ya wagombea kutoka
chama  cha mapinduzi CCM kufikia wawili akiwemo Mbunge wa jimbo hilo,
Wiliam Lukuvi ambaye bado ameonyesha nia ya kuendelea kuliongoza huku
kwa upande wa chadema mbunge wa viti maamulu Chiku Abwawo pamoja
makamu mwenyekiti wa bavicha Ole Sosopi

Monday, May 18, 2015

Stendi kuu mjini Iringa waanzisha timu ya mpira wa miguu ya KIBIKI FC

Kibiki azizungumza na kijana, fundi viatu wa mjini Iringa!



Na mwandishi wetu, Iringa
 
VIJANA wa stendi kuu ya mabasi ya mjini Iringa, wameanzisha timu ya mpira wa miguu ya ‘Kibiki Football Club’ili kuunga mkono harakati za mwanahabari wa gazeti la Uhuru na mzalendo, baada ya kutangaza nia kuwania jimbo hilo.
 

Katibu wa timu hiyo, Charles Manet alisema wameamua kuanzisha timu ya mpira wa miguu inayoitwa Kibiki, ili kuonyesha dhamira yao ya dhati katika kumsaidia kijana mwenzao.
 
“Yeye mwenyewe hakujua kama tumetumia jina lake kwenye timu yetu, tayari tumeshacheza mechi mbili tangu timu yetu ianze kuitwa Kibiki FC na tunatarajia kuendelea kucheza mechi za kirafiki, tukianza na timu ya Wambi ya stendi kuu ya mjini Mafinga,”alisema
 
Maneti alisema wamekuwa wakisafiri kwa kuchangishana fedha na kwamba tayari wamepata jezi seti moja, kutoka kwa wadau mbali mbali wa michezo mjini Iringa.
 
Aliwataka wapenzi wa soka la mjini Iringa kuunga mkono jitihada za vijana hao katika kuhakikisha, timu hiyo inasonga mbele badala ya kuikatisha tama.
 
“Pamoja na kukatishwa tama tangu tuunde timu hii lakini ukweli ni kwamba, hatutaacha kwa sababu Kibiki ni kiongozi na tusipomuunga mkono kijana mwenzetu tutakuwa hatujamtendea haki hata kidogo,”alifafanua.
 
Kabla ya kuunda timu hiyo vijana hao, walichangishana fedha zaidi y ash laki moja na kumkabidhi Kibiki, wakimtaka azitunze kwa ajili ya kuchukulia fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Iringa, muda ukifika.
 
Wakizungumzia ubunge, vijana hao walisema kuwa jamii ya wana Iringa inatarajia kumpata kiongozi anayetokana na wenyewe, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ili wampigie kura ya kuwa mbunge wa jimbo hilo na sio vinginevyo.
 
Tangu alipotangaza nia ya kuwania jimbo hilo, Kibiki amekuwa akikubaliwa na makundi mbalimbali wakiwemo vijana, walemavu, wanawake na wazee.
Mwisho.

Monday, May 4, 2015

KATIBU MKUU WA UVCCM SIXTUS MAPUNDA AHARIBU MIPANGO YA WAPINZANI MKOANI IRINGA



 katibu mkuu wa uvccm taifa sixtus mapunda akiwapa maneno ya kishujaa wakazi wa mkoa wa iringa
 juliana shonza akiwahutubia wananchi wa mkoa wa iringa
 viongozi chama cha mapinduzi wakiwa katika meza wakifuatia mkutano unavyoendele

na fredy mgunda,iringa.

katibu mkuu wa uvccm taifa afanya ziara ya jimbo la kilolo kwa lengo la kukijenga chama  na kuangalia maendeleoya chama hicho  hasa ngazi vijana lakini akiwa katika ziara hiyo aliongozana na mwenyeji wake   katibu wa uvccm mkoa wa iringa.

akihutubia wakati wa mkutano uliofanyika katika kijiji cha kitumbuka kata ya ilole katibu wa uvccm mkoa wa iringa elisha mwampashi aliwataka wanachama wa chama hicho kuondoa unyonge dhidi ya wapinzani wake kwa kuwaambia ukweli wananchi juu ya maendeleo yanayofanywa na chama hicho.

aidha mwampashe amesema kuwa ifike wakati viongizi wa chama hicho kuacha kujidanganya kwa kuwapa taarifa viongozi  za matumaini juu ya maendeleo ya chama hicho.
“tunatakiwa tubadilika sasa kwa kuwapa taarifa za ukweli viongozi wetu ili wanapoondoka wajue  nini cha kufanya ili kuondoa dosari ambazo zinzkuwa zikijitokeza,tuenaelekea kwenye uchaguzi mkuu ambao utafanyika hapo “alisema mwampashe

kwa upande wake katibu wa uvccm taifa  sixtus mapunda amewapongeza wananchi na wanachama wa tarafa ya ilole kwa ujumla  kwa ushindi walioupata wakati wa serikali za mitaa ambao unaashilia chama hicho kuendelea kupendwa kata tarafa hiyo.

lakini mapunda aliwatoa hofu wananchi wa kijiji cha kitumbuka kwa kusema amesikia na kujionea baadhi ya matatizo yanayoikabili kata ya ilole na kuwaahidi kuyafikisha kwa mbunge wao na kutafuta njia ya kuyatatua kwa kuwa profesa petter msola ni msikivu.

“tatizo la kufikisha nguzo za umeme katika eneo hili ni tatizo dogo ambalo linatatulika kwa haraka na kuwaahidi wananchi kulifanyia kazi mapema ,suala la barabara alisema kuwa amejionea yeye mwenyewe kuwa  si nzuri na inahatarisha maisha kwa kuwa pindi mvua itakaponyesha barabara hiyo itakuwa kama mto”.alisema mapunda.



ALIYEKUWA  kada maarufu  wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema ) Taifa Juliana Shonza ambae alijiuzulu na chama hicho na kijiunga na CCM amewataka wakazi wa jimbo la Iringa mjini kuungana kulipokea jimbo kutoka kwa mbunge Mch Peter Msigwa.

Shonza ametoa kauli hiyo leo wakati akiwahutubia wakazi wa jimbo la Iringa mjini wakati wa mkutano wa uzinduzi wa matawi unaofanywa na katibu mkuu wa Uvccm Taifa sixtus Mapunda.

Alisema jimbo la Iringa mjini ni jimbo ambalo wananchi walichagua mbunge kwa hasira na kuwa badala ya kutegemea maendeleo wamejikuta wakifanya maandamano yasiyo na kikomo kila uchwao.

Shonza alisema kuwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini amekuwa ni mtu wa kujipigania mwenyewe kimaisha badala ya kujishughulisha kuwaletea wananchi maendeleo.

Hivyo alisema ni vema wananchi wa Iringa mjini kujipanga kwa hafla ya kulipokea jimbo hilo kutoka kwa mpangaji mbunge Msigwa aliyepanga bila kujua kama kapangishwa hivyo kushindwa kulipa kodi.

Akielezea juu ya hofu ya muungano wa vyama vinavyounda katiba ya wananchi (ukawa) alisema kuwa Chadema ni chama ambachokinataka kupanda kupitia ukawa.

Kwani alisema Chadema ndio chama kilichokituhumu CUF kuwa ni CCM  B na kuwa ni chama cha kishoga imekuwa leo kuungana 

Hivyo kuwataka watanzania kupima na kutoa maamuzi magumu pindi uchaguzi utakapo fika.

Nae mjumbe wa kamati ya utekelezaji Uvccm Taifa Secky Kasuga alisema wananchi wa jimbo la Iringa walianzimisha jimbo hilo na sasa mwenye Nyumba anahitaji Nyumba Yake hivyo lazima mpangaji kuondoka.

"Tunalazimika kuchukua Nyumba yetu baada ya mpangaji kushindwa kufagia nyumba"

Katibu mkuu wa UVccm Taifa Sixtus Mapunda alisema kilio cha maendeleo kwa jimbo la Iringa kimetokana na mchanganyo uliofanywa na wananchi kwa kumchagua mbunge mrudisha nyuma maendeleo.

Alisema mbunge amekuwa kikwazo kikubwa kwani bungeni wakati wa vikao vya bajeti yeye anatoka nje ya bunge na wakati wa vikao vya kupanga shughuli za maendeleo halmashauri yeye anashiriki kuita maandamano.

" Tunawaombeni wana Iringa mtusaidie kurejesha jimbo kwa kumtoa mbunge mpinga maendeleo katika jimbo la Iringa mjini ambalo maendeleo yanaletwa kwa nguvu na ccm"

Bw Mapunda asema anawashangaa wapinzani kwa kuikataa katibu inayopendekezwa ambayo unazungumzia pia Haki ya kuishi hivyo  kupinga Kwao wanapinga hadi haki ya wao kuishi.

Alisema kuwa hoja Yao ni kutaka serikali tatu na si vinginevyo na kuwa wananchi lazima wapigie kura ya ndio katiba hiyo na pindi muda wa serikali tatu utakapofika basi itafanyika hivyo na si sasa.

Kuwa kuutaka utanganyika ni kuutaka ukoloni hivyo lazima kujitambua kuwa wakati wa kuongozwa na wakaloni umepita.





Friday, May 1, 2015

mkuu wa wilaya ya korogwe hafsa mtasiwa amewataka wananchi kuisoma na kuilewa katiba inapendekezwa

                        mkuu wa wilaya ya korogwe HAFSA MTASIWA
         mkuu wa wilaya ya korogwe HAFSA MTASIWA


na fredy mgunda,iringa

Wanachi wa mkoa wa tanga wilaya ya korogwe wametakiwa kuisoma na kuilewa katiba inapendekezwa ili waweze kuipigia kura.

Akizungumza na blog hii mkuu wa wilaya ya korogwe HAFSA MTASIWA awataka wananchi wa wilaya hiyo kusoma na kuijadili katiba hiyo na kutosikiliza kutoka kwa watu.

Aidha MTASIWA amesisitiza kuwa Tanzania bado tunakatiba yetu na tupo kwenye mchakato wa kupata katiba mpya hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini na maneno wanayo ambiwa na watu wengine.

“Katiba inayopendekezwa imeandikwa na binadamu wa kawaida kama ilivyokuwa hapo awari katika katiba ambayo inatumika hadi sasa lakini inapaswa kuangalia kuna mambo gani mapya ambayo yameandikwa kwenye katiba inayopendekezwa na imebeba mambo gani muhimu katika maendeleo ya Tanzania yetu”.alisema mtasiwa

Lakini MTASIWA ameendelea kuwataka watanzania kwa ujumla kuendelea kuidhamini amani tulivyo nayo kwa sasa na tusiwafuate wananchi wengi wenye lengo la kuvuruga amani yetu kwa maslai yao binafsi hivyo watanzania msidaganyike kwa maneno yao.

MTASIWA amewaomba wazazi wote kuwapa elimu ya kutosha watoto wao juu ya kutunza amani na kuacha tabia ya kushabikia maneno ya uchochezi yenye lengo la kuvuga amani yetu.

Wakati huohuo MTASIWA amewataka wananchi wa wilaya hiyo kujua umuhimu wa kutumia bima na wajitokeze kuchangia katika mifuko ya bima.

Bima ya afya inafaida kubwa sana katika maisha yako hivyo lazima wananchi watambue umuhimu wa kuchangia bima kwa kuwa serikali imepanga kuwachangia wananchi kwa kiasi kile ambacho wamekichanga kwa mfano wananchi wakichanga milioni 100 na serikali itatoa milioni 100 kwa lengo la kuboresha sekta ya afya.alisema MTASIWA.


MWISHO.




Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More