Thursday, April 23, 2015

KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA HASSAN MTENGA AENDELEA KUVURUNGA MIPANGO YA WAPINZANI KATIKA JIMBO LA ISMANI

 katibu wa CCM mkoa wa iringa HASSAN MTENGA akiwahutubia wananchi wa tarafa ya pawaga.
 katibu wa CCM mkoa wa iringa HASSAN MTENGA akijibu maswali ya wananchi wa tarafa ya pawaga.
katibu wa CCM mkoa wa iringa HASSAN MTENGA akiwapa vifaa vya michezo wananchi wa tarafa ya pawaga

na fredy mgunda,iringa

katibu wa chama cha mapinduzi  mkoa wa iringa hassani mtenga  amewataka wananchi wa tarafa ya pawaga katika jimbo la isimani kuendelea kumwamini mbunge wa jimbo hilo kwa kuwa anawatendea haki kwa kuwaletea maendeleo.

akizungumza katika mkutano huu  katibu wa chama hicho MTENGA  amewataka wananchi kuendelea kukiamini chama hicho kutokana na kutekeza ahadi zao ambazo wanakuwa wanaziahidi kwa wananchi.

Kwa upande wao wananchi kijiji cha boliboli kilichopo tarafa ya pawaga wilaya ya iringa vijijini  wanakabiriwa na matatizo ya kiafya pamoja na migogoro ya aridhi baina ya wafugaji na wakulima hayo yamebaini katika mkutano ulifanyika katika kijiji hicho.

wakizungunza wakati wa mkutano huo wananchi hao wamesema kuwa  kijiji hicho hakina mganga wa kutoa huduma katika zahanati yao na kuongeza kuwa tatizo la migogolo ya aridhi limekuwa kubwa.

Akijibu maswali ya wananchi hao katibu wa ccm mkoa wa iringa hassani mtenga  amewata  viongozi wa chama hicho kufanya mikutano ya mara kwa mara na kupokea kero za wananchi na kuzitatua mapema ili kuendelea kukijengea imani chama chao.

Viongozi wengi wamekuwa hawawajali wananchi wao ambao wamewaweka matarakani na ndio imekuwa sababu ya matatizo mengi na migogolo mikubwa katika vijijini.

Lakini MTENGA amesema swala mfureji,tatizo la mganga,walimu kuwa walevi na mgogoro wa mbomipa anayachukua na kwenda kuyafanyia kazi na kuwaahidi kuwa matatizo yote waliomweleza yatatulika.

“Alimalizia kwa kuwaomba wananchi kuipigia kura katiba inayopendekezwa ili waweze kupata katiba ya wananchi na kuwaambia wananchi wa eneo hilo kuitumia fursa ya kuijiandikisha katika daftari la kudumu la kupigia kura ambalo iringa litaanza tarehe 29 mwezi huu” alisema HASSAN MTENGA.

mwisho.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More