mwanahabari frank kibiki , aliyewahi kuwa katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa nec akiwa na watoto waliofanyiwa ukaliti wa kijisia pamoja mkuu wa kituo cha matumaini centre
mwandishi wa habari wa gazeti la mzalendo na uhuru TUMAINI MSOWOYA KIBIKI akiwa na watoto waliofanyiwa ukatili wa kijinsia
mwandishi wa habari wa gazeti la mzalendo na uhuru TUMAINI MSOWOYA KIBIKI akiwa na watoto waliofanyiwa ukatili wa kijinsia pamoja na mkuu wa kituo cha matumaini centre.
na fredy mgunda,iringa
Ukatili
wa kijinsia kwa watoto wa kike ndio inaonekana kuwa sababu ya mkoa wa iringa kuzalisha wafanyakazi wengi
wa kazi za ndani
akizungumza
na blog hii mwanahabari frank kibiki , aliyewahi kuwa
katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) ngazi ya wilaya kwa
zaidi ya miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa nec.amesema kuwa watoto wengi wa kike
hawapewi nafasi ya kwenda kusoma kutokana na tamaduni potofu hivyo waandishi wa
habari tunatakiwa kuungana kuwapigania watoto hawa.
Aidha
KIBIKI amewataka wananchi wa mkoa wa iringa kushirikiana na mkuu wa kituo cha
matumaini centre ili kuwasaidia watoto wa kike ambao wanaishi katika kituo hicho.
lakini
KIBIKI amewaomba viongozi mbalimbali na waandishi wa habari kupaza sauti zetu
ili kukomeshakabisha suala la ukatili wa kijinsia ambao bado unaendelea hapa
mkoani kwetu.
Wananchi mkoani iringa
wametakiwa kuwathamini na kuwapa elimu watoto wa kike ili kupunguza unyanyasaji
wa kijinsia unaoendelea kwa sasa.
Kwa upande wake mkurugenzi
kituo cha matumaini centre HELLEN NKUNDA amesema kuwa amekuwa akipokea watoto
wengi wa kike ambao wamefanyiwa ukatili wa kijinsia na amekuwa akiwapokea na kuwapa elimu ya
ufundi.
Lakini NKUNDA amewataka
watoto hao kuwa makini na waaminifu katika maisha yao ili wasirudie yale ambayo
yalimtokea hapo awali na wasikubari kudanganywa tena.
NKUNDA ameitaka serikali kutoa elimu kuanzia shule ya msingi juu
madhara ya ukatili ili kujenga jamii ambayo itakuwa na elimu juu ya unyanyasaji
na ukatili wa kijinsi hasa kwa watoto wa kike.
Alimalizia kwa kumshukuru
mwandishi wa habari frank kibiki kwa kutoa msaada wake kwa mtoto ambaye
aliyekuwa amefanyiwa ukatili wa kijinsia.
0 comments:
Post a Comment