
Kaimu mkuu wa wilaya Mufindi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richad Kasesela akitoa neno kwenye mkutano wa maombi ya kurekebisha bei ya umeme wa Mwenga Power Limeted katika kijiji cha Igoda kilichopo wilaya ya MufindiBaadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wa wadau wanaotumia umeme wa kampuni ya MwengaNa Fredy Mgunda,Iringa.MKUU wa wilaya ya Mufindi ameitaka kampuni ya Mwenga Power Services Limited kutengeneza mita za wateja zilizoharibika kwa wakati ili wananchi waendelee kufanya shughuli za kimaendeleo kwa kutumia nishati ya umeme ambayo inatolewa na kampuni hiyo.Akizungumza kwenye mkutano wa maombi ya kurekebisha bei za umeme zinazotolewa na kampuni ya Mwenga,kaimu mkuu wa wilaya hiyo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa,Richad Kasesela...