Na Fredy Mgunda,Irnga.Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo amesema kuwa wakandarasi watakao chelewesha au kujenga chini ya kiwango miradi ya kimaendeleo katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa watarudia kwa gharama zao kwa ubora ule ule unatakiwa kutokana na thamani ya mradi husika.Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua miradi ya kimaendeleo katika manispaa ya Iringa, mkuu wa wilaya Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa amefanikiwa kukagua miradi mingi ambayo imejengwa kwa viwango vinavyotakiwa ila tatizo kubwa lipo kwa wakandarasi ambao wamekuwa wakipewa tenda za ujenzi wa miradi hiyo.alisema kuwa wakati wa ziara aligundua kuwa wakandarasi wengi wameshalipwa fedha serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi ya serikali ila wamekuwa wanaichelewesha...